Monday, September 18, 2017

Be A Donor

"Pamoja Tunaweza"
Lengo letu kuu ni kuhakikisha watoto wanaosoma katika mazingira magumu kupata njia rahisi ya kufikia vifaa vya kujifunzia, kwa kuboresha mazingira ya shule. Tunatambua kuwa ili kufanikisha hili jambo tunahitaji NGUVU YA JAMII.



Thursday, September 14, 2017

DIRA YETU


..."Tumepiga hatua kubwa katika ndoto ya kuhamasisha umma kuhusu adha wanayopata wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini na kuungana nasi kukabili adha hiyo"..

Wednesday, September 13, 2017

JUHUDI ZA KUIMARISHA MAZINGIRA BORA


Tafadhali toa maoni yako, ni juhudi zipi zitumike kuimarisha mazingira bora ya kusomea kwa watoto wetu?


Monday, September 11, 2017

BE A DONOR


Our mission is to improve the quality of the classroom environment to make the school the best place to be for all students and to tap the maximum potential of every child, academically and physically through sports, drama, music and arts by creating conducive learning climate and for sports in schools.

So far we have helped over 30,000 students from our programs and project. we would never do this if it weren't for the support we got through partnership, donor, volunteering, individual supporters, corporate, local government and other stakeholders.

Our vision by 2020 is to seat 45,000 or more students on a desk,
  •  1000 teachers on basic furniture, 
  • 3000 Special Education Needs Pupils Seated on customized desks, 
  • 200 public schools to have essential furniture, 
  • 100 Pre-Primary Schools to have Reading Corners with basic books, 
  • 30 Public Primary Schools with basketball facilities including coaches. 
  • 300 girls &300 boys active in basketball game.
  •  50 Special Education Need Pupils have access basketball facilities & Coaches


Please contact us to become a DONOR

Tuesday, September 5, 2017

International Day Of Charity


Kila Mwaka, Misaada duniani kote husaidia kuokoa na kuboresha maisha ya watu, Kupamba na magonjwa na Kulinda watoto, na kutoa matumaini kwa maelfu ya watu. Ili kuheshimu kazi muhimu ambayo misaada hii mingi, Mwaka 2012 Umoja wa Mataifa uliamua kuteua siku ya kimataifa ya misaada kama siku rasmi ya kutambuliwa na sherehe. Sabau tarehe hiyo ilichaguliwa ni kwa sababu ya kumbukumbu ya Mama Teresa wa Calcutta, Uchaguzi huu unakumbuka kazi aluzofanya kwa kutoa Maisha yake kwa kazi ya Upendo. Ili kusheherehekea siku hii maalum kila mwaka, kazi ya misaada tofauti kila neno hutangazwa na kusheherekea na watu wanahimizwa kutoa mchango wa fedha na wakati kuganya kazi za misaada, na pia kuwaelimisha watu na kuongezza ufaham kuhusu watu wengi wa misaada duniani kote. Elimu y akutoa ni kiini cha siku hii Maalum. (Source: Dayof the Year website)
Jee! wewe umenitolea nini mwaka huu? 

Tafadhali wasiliana nasi kwa kujiunga na kampeni zetu

Hii Ndio Nguvu Ya Jamii

Pamoja tunaweza





Wednesday, August 23, 2017

Monday, August 21, 2017

HASSAN MAAJAR TRUST YAKABIDHI VITABU VYA KUSOMEA KATIKA SHULE YA SHIMBWE, KILIMANJARO





Makamu Mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust - Sharif Maajar akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe, Anne E Mghwira.



HOTUBA FUPI YA MAKAMU MWENYEKITI WA HMT KATIKA HAFLA SHULE YA SEKONDARI SHIMBWE – TAREHE 19 AGOSTI, 2017
Niko hapa kuwakilisha Hassan Maajar Trust, kwa kifupi, HMT; taasisi ambayo ilianzishwa mwaka 2011 kwa lengo kuu la kuchangia elimu bora katika shule nchini Tanzania. Mimi ni Makamu Mwenyekiti wa HMT. Ili kutimiza lengo hilo, tumekwa na mipango na miradi mbalimbali ya kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia.
Uhusiano wetu na shule hii ya Shimbwe Sekondari ni wa kipekee kabisa. Uwepo wetu hapa leo, ni mwendelezo wa historia yetu na shule hii ambayo ilianza wakati wa ujenzi wake miaka ya 70.
Wakati huo, Mwenyekiti wa HMT, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, alitumia likizo zake kujiunga na Wanafunzi wenzake kutoka shule mbalimbali kushiriki kufytua matofali ya kwanza yaliyojenga shule hii.
Huu ulikuwa ni mwanzo wa safari endelevu ya kuchangia na kurejesha kwenye jamii na hususan hapa Shimbwe Sekondari. Nasema hivyo kwa sababu, baada ya hapo, popote alipokuwa Balozi Maajar alitafuta misaada kuendeleza miundombinu na taaluma kwa ajili ya shule hii.
Juhudi hizi zilichukuwa kasi mpya baada ya kuanzishwa kwa Taasis ya Hassan Maajar Trust. Kupitia HMT, tuliweza kuwatambulisha mashirika mawili ya Kimarekani; Malaika Kids na Powering Potential ambao kwa kushirikiana na nasi walifadhili kitengo cha compyta hapa shuleni.  Malaika Kids walitoa laptop 10 na Powering Potential wakaweka programu maalumu ya kufundishia iitwayo ‘Rachel’ pamoja na kutoa mafunzo waalimu wa ICT.
HMT kwa upande wake iligharamia utengenezaji wa samani (meza 13 na viti 60) kwa ajili ya chumba cha compyuta.
Aidha, HMT iliwashirikisha, Vodacom Foundation nao wakatoa laptops 10 na compyuta 10 pamoja na mafunzo maalum kwa waalimu.
Tunaamini ni kwa historia hiyo ya kujivunia, ndiyo imepelekea uongozi wa shule kutujulisha na kutualika tushiriki hafla hii ya ufunguzi wa bweni. Nasi katika HMT tumeona ni heshma kubwa kwa taasisi yetu, hivyo tumeamua tusije mikono mitupu.
Tumeona pia kati ya mambo yanayoweza kuchangia elimu bora ni kujenga utamaduni wa kujisomea. Hivyo basi tumeleta vitabu kwa ajili ya kujisomea.
Kwa niaba ya Bodi ya Hassan Maajar Trust, naomba kuwasilisha mchango wetu huo.




















Friday, August 18, 2017

HASSAN MAAJAR TRUST NA RADAR EDUCATION WAKARABATI MAKTABA NA KUTOA VITABU 900 KWA SHULE YA MSINGI MAJIMATITU





HASSAN MAAJAR TRUST NA RADAR EDUCATION WAKARABATI MAKTABA NA
 KUTOA VITABU 900 KWA SHULE YA MAJIMATITU

Dar es Salaam, tarehe 17 Agosti, 2017: Hassan Maajar Trust kwa kifupi HMT, hivi karibuni iliadhimisha miaka sita ya juhudi za kuboresha mazingira ya Elimu nchini. Kwa kushirikiana na kampuni ya Radar Education imekarabati maktaba ya shule ya Msingi Majimatitu na kutoa vitabu zaidi ya 900. Hafla ya kukabidhi maktaba na vitabu ilifanyika katika shule ya msingi Majimatitu, Mbagala, wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa HMT Balozi Bertha Semu-Somi na Meneja Mkuu wa Radar Education Bw. Arthur Walden, walikabidhi maktaba hiyo na vitabu kwa Mwalimu Mkuu, Bw. Abdallah Mgomi. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaniva alikuwa Mgeni Rasmi.
Akiongea na Waandishi wa Habari jana, Balozi Semu-Somi alisema, " Hii ni mara ya tatu kwetu kuwa hapa Majimatitu. Mwezi Agosti 2015, HMT ilitoa msaada wa madawati thelathini (30), kwa ajili ya Kitengo cha watoto wenye ulemavu. Wakati wa kukabidhi madawati hayo, HMT ilishuhudia takribani asilimia 90% ya wanafunzi wakikaa sakafuni. Tuliazimia kuhamasisha uchangiaji kwa kuandaa matembezi ya hiari kwa ufadhili wa Bank M.
Kupitia matembezi hayo, HMT ilifanikiwa kuelimisha umma kuhusu uhaba wa madawati Majimatitu; wengi waliitikia wito na kusaidia. Aidha HMT ilitumia kiasi cha fedha kilichotokana na wakati wa matembezi kutengenezesha madawati 280 yenye kukaa wanafunzi watatu hadi wanne kila moja, na hivyo kunyanyua wanafunzi wapatao 850 kutoka sakafuni.

Katika kuchangia Elimu bora nchini HMT inalenga kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kusoma vitabu. Mwaka huu, kwa kushirikiana na Radar Education, tumeamua kuiwezesha shule ya Majimatitu kwa kukarabati maktaba na tumetoa vitabu zaidi ya mia tisa.
Bwana Walden wa Radar Education alisema; “Kwa kushirikiana na HMT katika mradi huu wa Maktaba, kwetu imekuwa ni fursa nyingine ya kuchangia Elimu Bora Tanzania. Kwa leo tumetoa jumla ya vitabu 933. Ni matumaini yetu kuwa Wanafunzi watatumia vema msaada huu na kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu.”


Miaka sita ya shughuli za HMT chini ya kauli mbiu ”Dawati kwa Kila Mtoto”, taasisi hii imefanikiwa kutoa madawati 9,000 ambayo yamenufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 hapa nchini;. (Rukwa, Njombe, Singida, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Kigoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dar es Salaam, na Kilimanjaro). “Tumepiga hatua kubwa katika ndoto ya kuhamasisha umma kuhusu adha wanayopata wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini na kuungana nasi kukabili adha hiyo. “aliongeza Balozi Semu-Somi.


















HASSAN MAAJAR TRUST & RADAR EDUCATION REFURBISHES LIBRARY AT MAJIMATITU PRIMARY SCHOOL

District Commissioner Temeke Hon, Felix Lyavina (Right) Mkurugenzi Executive Director Ambassadoor Bertha Semu-Somi -Hassan Maajar Trust (middle) and Temeke Manicipal Education Officer (Left) cutting the ribbon.
Dar es Salaam, 17th August 2017: Hassan Maajar TRUST (HMT) recently marked its sixth year anniversary by partnering with Radar Education to refurbish the Majimatitu Primary School library along with a 933 books donation. The event was held at the school located in Mbagala, Temeke District, Dar es Salaam.
The HMT Executive Director, Ambassador Bertha Semu-Somi and Radar Education General Manager Arthur Walden on behalf of their organizations presented the refurbished library and books to Majimatitu Head Teacher, Abdallah Mgomi. The Temeke District Commissioner, Felix Lyaniva, officiated at the Event.
Speaking at the event yesterday, HMT’s Executive Director said, 
“This is our third time at Majimatitu.
 In August 2015, we donated 30 desks for pupils with disability. 
Then we found that 90% of students sit on the floor due to lack of desks. 
Committed to solve the problem and sponsored by Bank M, 
HMT organised a Charity Walk in November 2015”.
Through the Charity Walk, HMT succeeded in
 1) raising awareness on the shortage of desks at Majimatitu.
 Many Education Stakeholders heeded the call”.
 2) Collecting funds enough to procure 280 desks that sit three to four students each,
 thereby lifting over 850 students off the floor on to desks. 
HMT’s core objective is to contribute to an improved learning environment for
 quality education in schools. “We are delighted to have Radar Education on board this project.
The Radar Education Chief, Mr Walden stated “We are happy to join HMT for this Library project, which is for us a welcome opportunity to continue to contribute to quality Education in Tanzania.  We donated over 900 books. We hope that students will embrace this support aimed at building the culture of reading”
The renovation of this library is a part of HMT’s ‘A Desk For Every Child’ campaign, In six years, the Trust prides in over 9,000 desks donated to 13 regions (Rukwa, Njombe, Singida, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Kigoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dar es Salaam and Kilimanjaro) lifting over 30,000 students off the floor.
“We have gone far in realizing HMT’s dual dream of raising awareness on the plight of pupils learning to read and write while seated on the floor, and mobilising the public to join the HMT led initiative to resolve the problem’, added Ms. Semu-Somi.